Meneja wa kikosi hicho, Philip Alando, alisema kwa sasa wanaziangalia Simba na Yanga, jinsi zinavyofanyiana fitina na wao wanakimbiza mwizi kimya kimya.
“Wao (Simba na Yanga) wanafanyiana kila aina ya fitina ili mmoja wao aweze kupoteza mchezo, lakini kwa upande wetu hatuna neno na mtu na badala yake tunapambana kimya kimya na mwisho wa siku watashtuka tupo juu,” alisema.
Azam wametwaa ubingwa mara moja katika msimu wa 2013/14, tangu ilipopanda daraja msimu wa 2008, wamepania kuwazidi kete Simba na Yanga.
Katika msimamo wa ligi hiyo, Simba, Yanga, Azam FC na Mtibwa Sugar wana pointi 16 lakini wekundu hao wa Msimbazi wakiongoza kutokana na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Timu hizo nne pia hakuna hata moja ambayo imepoteza mchezo wowote, kitu ambacho kinaashiria kwamba msimu huu ni ngumu na Azam wametamba kwamba watawashushia kipigo kizito Ruvu Shooting ili kupanda rasmi kileleni.
0 comments:
Post a Comment