Image
Image

Kiungo Mtibwa Sugar ahamishia hasira Ndanda Fc.

KIUNGO mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, amesema kitendo cha kushindwa kuibuka na ushindi katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida United, kimewaudhi na sasa hasira zao zote wamehamishia kwa Ndanda FC.
Mtibwa Sugar ambao wanashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 16, watakuwa na kibarua ugenini mkoani Mtwara, kumenyana na Ndanda ‘Wanakuchele’ Jumamosi hii.
Akizungumza na BINGWA jana, Issa alisema wachezaji wote wana hasira za kukosa pointi tatu dhidi ya Singida United, ambazo zingewapeleka kileleni na sasa wako kamili kuivaa Ndanda.
“Naamini tunakwenda kuchukua pointi tatu Mtwara ili tuweze kutimiza malengo yetu, ambayo tumejiwekea msimu huu, mchezo wetu uliopita dhidi ya Singida United, tulidhani tutashinda, lakini hali ikawa tofauti hivyo tunataka kurekebisha makosa,” alisema Issa.
Alisema anauheshimu uwezo wa Ndanda, kwani ni timu nzuri lakini lazima wakubali kupoteza mchezo huo ili waendeleze rekodi yao ya kutokupoteza mchezo.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment