Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imesisitiza juu ya tahadhali iliyotolewa ya uwepo mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya nchi na kusema ni vema wananchi wakachukua tahadhari hasa wanaoishi mabondeni.
Utabiri wa TMA bado unaonesha uwepo wa mvua kubwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia Novemba 1 mwaka huu na kwamba dalili zote zinaonyesha Dar es Salaam kukubwa na mvua hizo.
TMA imesema ni muhimu tahadhari zikachukuliwa kwa umakini ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza hasa katika mikoa inayotarajiwa kuwa na mvua kubwa kwa siku tatu kuanzia Novemba 1 ambayo ni pamoja na Tanga, Pwani, Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment