Serikali imesema inaandaa mwongozo wa msamaha wa matibabu kwa watu wenye ulemvu wakiwemo watu wenye Ualbino.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Vijana ,Ajira na Walemavu Mh Stella Ikupa wakati akijibu swali la Mh Mgeni Kadida mbunge wa viti maalum ambaye alitaka kujua kama serikali ipo tayari kuondoa kodi katika mafuta ya ngozi kwa watu wenye Ualibino.
Mh Ikupa amesema serikali inatambua changamoto zinazowakabili watu wenye Ualbino na imechukua hatua kadhaa ikiwemo kusambaza vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na watu wenye Ualbino.
Akaongeza kuwa katika mwaka 2016/2017 serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknlojia na Elimu ya Ufundi imesambaza miwani ya jua.
Aidha Mh Ikupa akasema kuwa tayari BohariKuu ya Dawa Nchini MSD imejumuisha katika orodha ya madawa,mafuta kinga kwa ajili ya kuzuia miale ya jua kwa watu wenye Ualibino.
Naibu Waziri akaongeza kuwa mafuta hayo hutolewa bure bila ya malipo katika hospital za serikali hapa nchini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment