Image
Image

Ndugai: Sitambui kujiuzulu kwa Nyalandu.

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesisitiza kuwa bado barua ya kujiuzulu nafasi ya ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu haijafi ka rasmi ofi sini kwake, hivyo anamtambua kiongozi huyo kuwa bado ni mbunge.
Ndugai aliyasema alipozungumza kwa njia ya simu na gazeti hili, kuhusu kama ofisi yake imeipata barua hiyo na hatua zinazochukuliwa baada ya mbunge huyo kujiuzulu ubunge na kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Yaani haya mambo mie ninayasikia kwenu tu (waandishi wa habari) na kwenye vyombo vya habari. Sisi kama Bunge mpaka sasa hatuna rekodi yoyote ya Mheshimiwa Nyalandu kujiuzulu nafasi yake ya ubunge,” alisisitiza Ndugai.
Aidha, alionesha kushangazwa na kitendo cha Nyalandu kuchukua uamuzi kujitangaza kwa vyombo vya habari kujiuzulu nafasi yake ya ubunge na kuhama chama kabla ya kuwasilisha barua yake rasmi kwa ofisi ya Bunge.
“Kwa maana rasmi mpaka sasa (jana mchana) mimi kama Spika sitambui kujiuzulu kwa Nyalandu, na ninamtambua kuwa bado ni mbunge wa Singida Kaskazini, na hata akija katika Bunge lijalo, nitampokea kwa mikono miwili hadi pale nitakapopata rasmi barua yake,” alisisitiza.
Nyalandu juzi alitangaza mbele ya waandishi wa habari jijini Arusha, kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama ya CCM ikiwemo ujumbe wa Halmashauri Kuu na kukiomba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumpokea kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa hali ya siasa nchini.
Alisema tayari amemwandikia Spika wa Bunge Ndugai, barua ya kujiuzulu nafasi yake ya ubunge aliyoitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2000 hadi sasa.
Kwa upande wake, Chadema kupitia Katibu wake wa Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema wako tayari kumpokea Nyalandu kwa mikono miwili kama nafsi yake itakuwa ni ya kweli, lakini endapo itakuwa na dhamira ovu atajikuta akibaki peke yake.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment