Image
Image

"Uchochezi na Takwimu za kupikwa" sababu za kukamatwa zitto Kabwe.

KAULI za uchochezi na kukiuka sheria za mtandao na takwimu, zimemfanya Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto kukamatwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa katika vituo viwili tofauti vya Polisi na kuachiwa kwa dhamana hadi wiki ijayo.
Aidha, Zitto akizungumza mara baada ya kuachiwa kwa dhamana akiwa kituo cha Kamata, alisema wanachosubiri kwa sasa ni suala hilo kupelekwa mahakamani ambako ndiko sehemu pekee anayoweza kujitetea.
Zitto alikamatwa kwa mara ya kwanza asubuhi jana nyumbani kwake Masaki mjini Dar es Salaam na kupelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe ambako alihojiwa kwa saa kadhaa kwa uchochezi, kabla ya kuachiwa kwa dhamana ya watu wawili na kutakiwa aripoti kituo cha Polisi cha Chang’ombe Jumatatu ijayo.
Anadaiwa kutoa kauli za uchochezi kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani kata ya Kijichi, kwa kuwakataza wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali ya CCM imeshindwa kuwakamata waliompiga risasi Lissu pamoja na kushindwa kujua chanzo cha maiti mbalimbali zinazookotwa katika ufukwe wa Coco Beach.
Tundu Lissu ni Mbunge wa Singida Mashariki ambaye alipigwa risasi hivi karibuni mjini Dodoma na kujeruhiwa ambapo hadi sasa anapatiwa matibabu Nairobi nchini Kenya. Akizungumza Wakili wa Zitto, Stephen Mwakibolwa alisema sababu zilizofanya akamatwe ni kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezi.
Akiwa kituo cha Polisi Kamata, Zitto alihojiwa kwa tuhuma mbili ambazo ni kuchapisha takwimu za serikali juu ya hali ya uchumi wa nchi kusinyaa ikiwa ni kinyume na Kifungu cha 37(5) ya Sheria ya Takwimu 2015.
Tuhuma za pili kwa Zitto ni kusambaza taarifa hiyo ya Uchambuzi ya Takwimu ya Kamati Kuu ya ACT Wazalendo kwenye mitandao ya Kijamii kinyume na Kifungu cha 16 cha Sheria ya Mitandao ya Kijamii (Cyber Crime Act).
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alithibitisha kukamatwa kwa Zitto jana asubuhi nyumbani kwake na kupelekwa Kituo cha Polisi Chang’ombe kwa mahojiano kutokana na kutoa kauli za kichochezi katika mkutano wa kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani wa Kijichi wilayani Temeke.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Kamanda Mambosasa alisema baada ya kuhojiwa Chang’ombe, baadaye alikamatwa na kupelekwa kwa DCI. “Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam tulimuachia Zitto kwa dhamana mchana, lakini alikuwa anatafutwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa kosa la kutoa taarifa za takwimu zisizo sahihi ambapo ni kinyume cha Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015,” alisema.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment