Tannesco yafanya operesheni maalum Dar es Salaam,
yanasa wanaohujumu shirika hilo.
Shirika la umeme nchini Tanesco limefanya operesheni
maalumu katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam lenye lengo la
kuwabaini wale wote wanaoiba umeme na kufanikiwa kukamata zaidi watu kumi.
Operesheni hiyo iliyo ongozwa na timu ya wakaguzi
kutoka makao makuu ya shirika hilo chini ya mkuu wa msafara Mhandisi mkuu Mposhe
Leye Zawadi ambaye alisema wote waliobainika watafikishwa Mahakamani kujibu
tuhuma zao na kwasasa wanashikiliwa na polisi.
Kwa upande wake meneja wa Tanesco mkoa wa Temeke amesema
pamoja na kufanya operesheni hiyo pia amewataadharisha wateja hao kuacha mara
moja kuepuka kutumia vishoka kuwaunganishia umeme bila kufata taratibu za
shirika hilo.
Watuumiwa wakiwa chini ya ulinzi Wa jeshi la polisi.
0 comments:
Post a Comment