Image
Image

Mlinzi Tanesco adaiwa kuua mwenzake, Polisi kufanya uchunguzi kubaini ukweli.

Jeshi la Polisi mkoani Mara linafanya uchunguzi wa tukio la kuuawa mlinzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), David Komoko (30) kwa kupigwa risasi ndani ya bohari ya shirika hilo mjini Musoma.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mara, Emmanuel Kachewa, alisema tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita saa 10.30 usiku.

Kachewa alidai kuwa mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya Jirani Security Group, Analias Katesi alimpiga risasi mlinzi mwenzake na kufariki dunia hapo hapo.

“Chanzo cha mauaji hayo ni baada ya Katesi muda wa usiku akiwa lindoni kuona watu wanne ndani ya uzio wa bohari, umbali wa mita 100 hivi, na kati ya watu hao mmoja wao alikuwa amebeba mzigo kichwani,” alidai.

Alidai baada ya kuwatilia shaka, aliamua kumfyatulia risasi mtu huyo aliyekuwa amebeba mzigo ambao ulikuwa ni vifaa mbalimbali vya umeme na thamani yake haijafahamika.

Kachewa alidai baada ya Katesi kumsogelea, alibaini mtu aliyepigwa risasi ni miongoni mwa walinzi waliokuwa wakilinda bohari tena  akiwa amevalia sare za kazi za shirika hilo hilo.

Alidai kuwa eneo ambalo marehemu alikutwa, jirani yake kulikuwa na tundu kubwa ambalo inadaiwa ndipo wezi walipopita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki alipotafutwa kuzungumzia suala hilo hakupatikana, lakini habari kutoka ndani ya jeshi hilo zinasema Katesi anashikiliwa kwa mahojiano.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment