 |
| Mbaraka Haji Batenga - Kaimu msemaji idara ya uhamiaji |
Idara ya uhamiaji inawashikilia watu watatu wanaodaiwa kuwa matapeli wakutisha ambao wanajishughulisha na utengenezaji wa hati za kusafiria, vibali vya ukaazi pamoja na mihuri 56 ya idara zote nyeti za serikali ikiwemo, Mabenki, Ikulu,Vizazi na Vifo sambamba na stakabadhi za malipo ya serikali.
Kaimu msemaji wa idara ya uhamiaji Mbaraka haji batenga, amewataja watu hao kuwa ni BENEDICTO RWEIKIZA au Masuti, JANUARY MUTEMBEI na BENETTY MTATIRO ITANG"ALE, huku wakiwa na vibali bandia ambavyo tayari vimetengenezwa kwa raia wa china vyenye thamani ya shilingi milioni 45.
 |
| Muhuri Bandia |
 |
| Mihuri Bandia |
 |
| TAPELI |
 |
| TAPELI |
 |
TAPELI Amesema mihuri mingine iliyokamatwa haina tofauti na ile halali ni pamoja na TRA,manispaa ya ilala, temeke, kinondoni, mawakili pamoja na misikiti na makanisa kwa ajili ya kutengenezea hati za vifo na ndoa. |
Aidha ameongeza kuwa watu haoambao ofisi zao zipo jirani na ukumbi wa bilicanas eneo la posta jijini Dar es Salaam wamekuwa wakijishughulisha na na biashara hiyo ya utapeli na kugushi hati na kwenda idara ya uhamiaji kuhakiki ili kuepuka usumbufu iwapo maafisa wa idara watakapoanza kazi ya kukagua vibali vya ukazi kwa wageni.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment