Image
Image

EXCLUSIVE: DK. BILAL AWATAKA WATANZANIA KUFANYA KAZI KWA BIDII ILI KUPAMBANA NA UMASIKINI.


Makamu wa rais Dr.Mohamed gharib Bilal amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kupambana na umasikini ili kujiletea maendeleo.

Dr.Mohamed gharib Bilal
Akizungumza wakati akifungua semina ya siku mbili ya utafiti wa kiuchumi na maendeleo iliyoandaliwa na taasisi ya Utafiti wa kiuchumi na maendeleo REPOA ,Dk Bilal amesema kazi ya serikali ni kuhakikisha inajenga mazingira na miundombinu itakayosadia mwananchi kushiriki ktk uchumi na maendeleo.

Amesema dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025 pamoja na mambo mengine inalenga kutumia rasilimali za taifa ktk kukuza uchumi ,kuboresha huduma za jamii ,kuongeza ajira pamoja na kuondoa umasikini kutoka kwa wananchi.

Prof.SAMWEL WANGWE - Mkurugenzi Mtendaji REPOA



Prof.Ibrahim Lipumba - Mchumi



Washiriki katika semina ya Masuala ya utafiti wauchumi wakifurahia jambo
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa REPOA Prof.SAMWEL WANGWE pamoja na balozi wa uholanzi hapa nchini Dr.AD KOEKKOEK wamezungumzia umuhimu wa kuinua uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja kupitia njia ya ujasiriamali kama ilivyofanyika ktk nchini nyingine  duniani.

Aidha Prof.Lipumba ambaye ni Mchumi amesema kukua kwa uchumi wa nchi kunatakiwa kuwapo ongezeko la maisha bora kwa wananchi lakini hali imekuwa tofauti hivi sasa ambapo zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wanaishi chini ya dola moja kwa siku.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment