Image
Image

EXCLUSIVE: WANANCHI MKOANI MARA HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MILIPUKO.

Wananchi wa serengeti mkoani - Mara


Na: Agustine Mgendi.

Wananchi wa Mji wa Mugumu wilaya ya serengeti mkoani mara wameulalamikia Uongozi wa Halmashairi ya wilaya hiyo kwa kile kinachodaiwa kushindwa kushughulikia tatizo la maji yanayosambazwa katika mji huo kutokana na kuwa machafu hali inayohatarisha afya zao.

Wakizungumza kwa Nyakati tofauti  Wakazi hao, Moses Juma na Chamba Ndogo wamekiri kupatikana kwa Maji katika mji huo ingawa si safi na Salama na hivyo kuibua hisia za kuibuka kwa Magonjwa mbali mbali ya milipuko na pia wakiwataka Viongozi wa Halmashauri hiyo na wale wa ngazi ya Kitaifa kuhakikisha maji hayo yanakuwa katika ubora wa kutumika.

Hata hivyo tatizo la maji safi na salama katika wilaya ya serengeti linatokana na shughuli za kibinadamu katika Bwawa la Maji la Manchira ambalo ni chanzo kikuu cha maji wilayani humo na hivyo kuhitajika uboreshaji Miundombinu hiyo ya maji.

Aidha kwaupande wake Mhadisi wa Maji wa Wilaya hiyo amesema ilikupata maji Safi na Salama katika halimashauri ya Wilaya ya Serengeti zinahitajika Shilingi bilioni 17, kwalengo la utengenezaji wa kiwanda cha kutibu maji, Huku kaimu mkuu wa wilaya ya serengeti Joshua Mirumbe akisema kwa sasa kuna changamoto kubwa ili kuhakikisha maji hayo yanakuwa katika ubora.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment