Image
Image

EXCLUSIVE: JESHI LA POLISI NCHINI TANZANIA LAWAPONGEZA WANANCHI KWA KUPUUZA MESEJI ZA VITISHO KWENYE SIKUKUU YA PASAKA.

Jeshi la polisi nchini tanzania limewapongeza wananchi kwa kupuuza meseji za vitisho waliokuwa wakitumiwa na baadhi ya watu kwa lengo la kuwatia hofu ili washindwe kuendelea na shughuli zao kwa kuhofia usalama wa maisha na mali zao hususani katika kipindi cha sherehe za sikukuu ya Pasaka mwaka huu.
ASP Advera Senso - Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania
Akizungumza jijini Dar es Salaam, nsemaji wa jeshi la polisi ASP Advera Senso ambapo ametoa wito kwa jeshi hilo kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kutoa taarifa za uhalifu, pamoja na wahalifu mapema kabla uhalifu haujatendeka katika eneo husika, huku akiwataka wananchi hao kuzingatia ushauri na namna ya  kujilinda na vitendo vya kihalifu na hatimaye kuzuia vyanzo vya uhalifu kwenye maeneo ya makazi wanapo ishi watu.


Aidha jeshi hilo limesema kuwa suala la jambo hilo  halikuwa na ukweli wowote hali iliyowezesha wananchi kusherehekea sikukuu yao vizuri kwa amani na utulivu.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment