Image
Image

EXCLUSIVE: LIGI KUU VODACOM YAINGIA RAUNDI YA ISHIRINI NA TANO

Ligi kuu ya vodacom (VPL) inaendelea katika raundi ya 25 kesho kwa mechi 5 zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Turian, Morogoro na Mlandizi IKiwa ni siku ya meimosi.

Ingawa yanga imetawazwa kuwa mabingwa wa VPL msimu huu 92012/2013), mechi dhidi ya Coastal union itakayochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam itakuwa ni moja kati ya mechi za kusisimua zitakazo wakusanya mashabiki wa mpira wa miguu nchini kushuhudia kitakachokuwa kikiendelea.

Mechi hiyo namba 172 itachezeshwa na mwamuzi Simon Mbwerwa kutoka Pwani akipewa sapoti na Said Mnonga na Charles Chambesa wote wakiwa wa mtwara huku mwamuzi wa mezani akiwa ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam, Kamishna wa mechi hiyo Davidi Lugenge Kutoka Mkoani Iringa.


Mtwibwa sugar itakuwa Mwenyeji wa wa African lyon Katika mechi Namba 170, itakayo chezeshwa na mwamuzi Dominic Nyamisana wa Dodoma kwenye uwanja wa Manungu huko turiani morogoro.

Na kagera sugar iliyo kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye uwanja wa jamhuri morogoro.

Aidha uwanja  Azam Complex ulioko chamanzi Dar es Salaam ukotayari kwa mechi ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons ambapo uwanja huo unauwezo wa kuingiza watazamaji 7,000.

Na Ruvu shooting itakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Mabatini ulioko mlandizi Pwani kuikabili Oljoro JKT kutoka arusha.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment