Image
Image

MAUAJI BUTIAMA YAKITHIRI,MWANAMKE AKATWA KICHWA


Na Augustine Mgendi, Mara.

Vitendo vya Mauaji Kwa Wanawake katika wilaya ya Buiama Mkoani Mara bado Vinaendelea baada ya Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Regina Manyama Mkazi wa Kijiji cha Nyakiswa kata ya Kyanyari wilayani humo kuuawa kwa kuchinjwa Kichwa na Watu wasiojulikana.

Mauaji Ya mwanamke kutenganishwa kichwa na kiwili wili Mara
Akiongea wakati wa Mazishi ya Mwanamke huyo,Mkuu wa wilaya ya Butiama mkoani Mara Bi. Angelina Mabula amesema kuwa vitendo vya Mauji katika wilayaa hiyo vinaendelea kuitia doa wilaya hiyo yenye historia kubwa hapa nchini.

Bi. Angelina Mabula - Mkuu wa Wilaya Butiama Mkoani Mara.
Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Butiama Bi Mercy Marambo na katekista wa kanisa Katoriki kigango cha Kiabakari Yohana Julius wamesema vitendo vya kuuwawa kikatili wanawake maeneo mbalimbali wilayani humo vinatakiwa kukomeshwa.

Vitendo vya Mauaji  wilayani humo vimekuwa vikitokea Mara kwa Mara ambapo wananchi mbalimbali wamekuwa wakiitaka Serikali kupambana na Mauaji hayo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment