Na.Emmanuel Msigwa , Tunduru
Wimbi la vitendo vya ujangili dhidi ya Tembo katika Pori la Selou la Tunduru Mkoani Ruvuma ambalo limekithiri siku za hivi karibuni limesababisha tembo wengi kukimbia kwenye makao yao msituni na kwenda kwenye makazi ya watu na kusababisha maafa mbalimbali wilayani humo ikiwemo ya kushambulia mashamba ya mazao na kuua watu wawili.
Tembo |
Kutokana na maafa hayo Mkuu wa wilaya ya Tunduru, CHANDE NALICHO akaongoza kikosi cha askari wa wanyapori pamoja na wananchi kuendesha zoezi la kufukuza Tembo hao katika maeneo yaliyoathiriwa huku akiwatoa wasiwasi wananchi kwamba Serikali imejipanga vyema na tayari vikosi vya wanyamapori vipo lindoni kupambana na Tembo waharibifu.
0 comments:
Post a Comment