Na. Munir Zakaria, Zanzibar.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mkusa Isaack Sepetu leo ameyatupa maombi yaliyofunguliwa na mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Evarist Mushi dhidi ya ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar(DCI), kutokana na kufunguliwa kinyume na sheria za Zanzibar.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo, Omar Mussa Makame alifungua maombi hayo, kupitia Mawakili wanaomtetea kupinga kitendo cha Jeshi la polisi, kumkamata na kushindwa kumfikisha mahakamani ndani ya saa 24, tangu Machi 17 hadi April 5 alipofikishwa Mahakamani.
Omar Mussa Makame Mtuhumiwa wa Mauaji ya Padri Mushi |
Kuhusu kesi ya msingi, upande wa mashtaka ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali, Abdallah Issa Mgongo, ameiambia Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo, bado haujkamilika na kuomba Mahakama kupanga tarehe nyingine ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Marehemu Padri Mushi |
Kwa upande wake, Jaji Mkusa amesema Mahakama haitakiwa kugeuzwa kama gurudumu la gari, kurudia mambo yaliyokwisha tolewa maamuzi na kuwataka kufika mahakamani kwa wakati, pamoja na kuwataka mawakili hao kubadilishana taarifa za mwenendo wa kesi hiyo ili kuepukana na vitendo vya kujadili mambo yaliyokwisha jadiliwa na kuamuliwa.
Mtuhumiwa Omar Mussa Makame ameshtakiwa kwa tuhuma za kumuua Padri Evarist Mushi wa kanisa katoliki, mnamo Febauri 17 kwa kumpiga risasi wakati akienda katika kazi ya utumishi wa Mungu huko katika kanisa la Mtakatifu Theresia liliopo Beitrasi mjini Zanzibar.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 9 mwaka huu, ambapo Jaji Mkusa amezitaka pande zote mbili kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia wakati, hususana suala la upelelezi kukamilika katika muda muafaka ili kesi iweze ianze kusikilizwa na kutolewa hukumu kwa mujibu wa
0 comments:
Post a Comment