Baada ya Mbunge huyo kuachiliwa huru, umati wa wanachama wa Chadema waliokuwa wamejazana katika Mahakama hiyo walifanya maandamano makubwa kwenda katika Ofisi za Chama hicho zilizopo maeneo ya Ngarenaro.
Lema akishuka kwenye gari ya polisi, pembeni akiwa askari. |
Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa "Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off.
Lema akiwa juu ya gari Baada ya kuachiwa Huru. |
Kosa la tatu ni pale alipotamka kwa wanafunzi kuwa "Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa Mkuu wa Mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadam
0 comments:
Post a Comment