Image
Image

BALE ASHINDA TUZO ZA MCHEZAJI BORA


GARETH BALE amefanikiwa kushinda tuzo mbili za mchezaji bora wa mwaka wa chama cha wacheza soka la kulipwa nchini England na mchezaji bora mwenye umri.



Winga huyo wa Wales na Tottenham Hotspur alishinda tuzo hiyo mwaka 2011 - ni mchezaji wa tatu kushinda tuzo hizo mbili kwa pamoja baada ya Cristiano Ronaldo mwaka 2007 na Andy Gray aliyefanya hivyo mwaka 1977. 

Winga huyo wa Spurs ambaye anawaniwa na timu nyingi barani ulaya alisema:  “Ni heshima kubwa, Kuchaguliwa na wachezaji wenzio ni jambo kubwa katika mchezo huu. Ni jambo kubwa kushinda na nina furaha sana. 

Unapoangalia washindani waliokuwa kwenye listi unashangazwa, lakini nisingeweza kuwashinda bila msaada wa timu yangu.

“Wamekuwa na msaaada mkubwa msimu huu - pia kocha wangu AVB - nisingeweza kushinda bila wao, ningependa kuwashukuru sana.

“Washindani wote wamekuwa na msimu mzuri sana watu kama Van Persie na Suarez.

“Siku zote nimekuwa nikiwapenda wachezaji kama Giggs na Thierry Henry, nimekuwa huku nikiwatazama wakicheza soka, kwa kuangalia mechi zao na hata wakiwa na wanapokea tuzo kama mimi leo - hivyo kuwa hapa usiku leo ni ndoto iliyokamilika.”

Bale amewashinda wachezaji wenzie Van Persie, Suarez, Carrick, Hazard na Mata.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment