![]() |
| Edward Lowassa - Waziri Mkuu Mstaafu Tanzania. |
Na Faraja Kihongole
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa amewakumbusha Watanzania kuzingatia umoja na mshikamano na kuepuka viashiria vya uvunjifu wa amani.
Akikabidhi Msaada wa Shilingi Milioni Tano kwa Baraza la Misikiti Tanzania BAMITA, kufuatia maombi ya Baraza hilo ya Ujenzi wa Chuo kitakachotoa Elimu ya Afya na Udaktari, ambacho kinajengwa katika kijiji cha Mengwa wilaya ya Kisarawe.
Amesema Tanzania imekuwa ni nchi ya mfano katika masuala ya mashirikiano baina ya dini tofauti miongoni mwa wananchi wake, hivyo kila mtanzania anawajibu wa kukemea na kujiepusha na dalili zozote zinazoonyesha kuwa lengo lake ni kuleta chuki za kidini.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa BAMITA Juma Kasim amesema fedha hizo zilizotolewa kwa ajili ya kendeleza ujenzi wa chuo hicho ambacho hadi kukamilika kwake kitahitaji zaidi ya Shilingi Billion moja, zitatumika kwa ajli ya kununua milango na madirisha kwaa jili ya vyumba viwili.
Katika hatua nyingine, bwana Lowassa amewaomba Waandishi wa Habari kuwa mabalozi wa kwanza katika kutangaza amani ya nchi.


0 comments:
Post a Comment