![]() |
| Utoaji wa Tuzo za (EJAT) 2013. |
TFF inawapongeza kwa ushindi huo uliotokana na makala zao ambazo zina mchango mkubwa katika maendeleo ya mpira wa miguu, na kutoa wito kwa waandishi zadi kutumia changamoto hiyo kushiriki katika kukuza michezo na hatimaye kufichua maovu yanayojitokeza kama vile Rushwa kwenye sekta hiyo hususani mpira wa miguu.
Hata hivyo waandishi waandishi waliokuwa wameshinda katika Kategori ya Michezo na utamaduni alikuwa ni Abdul Mohammed wa Mwananchi, Pamoja na Abdallah Majura wa radio ABM kwa upande wa radio.
Aidha katika hatua nyingine TFF imeipongeza timu ya Azamu FC kwa kufanikiwa kusonga mbele kwenye raundi ya pili ya michuano ya kombe la shirikisho baada ya kuitoa timu ya Barrack Young Controllers ya Liberia katika mchezo wa mwisho mwa wiki.
![]() |
| Azam FC |



0 comments:
Post a Comment