Image
Image

EXCLUSIVE: TUZO ZA UMAHIRI WA UANDISHI WA HABARI NCHINI TANZANIA ZAPATA MDHAMINI.


Aggrey Mareale - mwenyekiti na afisa mtendaji mkuu wa Excecutive Solutions (kushoto) akiwa na mwandishi 


Kampuni ya EXECUTIVE SOLUTION imetangaza kudhamini TUZO za Umahiri wa uandishi wahabari Tanzania(EJAT) kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa mwaka wa pili sasa mfululizo.















Mapema leo akikabidhi hundi ya shilingi milioni tatu kwa katibu mtendaji wa MCT,Kajubi Mukajanga,mwenyekiti na afisa mtendaji mkuu wa Excecutive Solutions,Aggrey Mareale amesema kampuni yake imeamua tena kudhamini tuzo hizo kwa kuthamini na kutambua kazi kubwa inayofanywa na Waandishi wa Habari.

Mareale amesema kampuni yake itaendelea kudhamini vipengele vya uchumi na biashara,afya,michezo,mawasiliano na teknologia,elimu,na mpiga picha bora.

Hata hivyo amelipongeza baraza la habari Tanzania kwa kuandaa tuzo hizo huku akisema hicho ni kichochea mojawapo kwa waandishi wa habari kuongeza bidii katika kazi na kuzingatia maadili na taaluma ya kazi hiyo.


Kajubi Mukajanga - katibu mtendaji wa MCT





















Akipokea hundi hiyo Mukanjanga ameipongeza Executive Solutions kwa kuthamini kazi za waandishi wa Habari na kushiriki katika tuzo hizo kwa mwaka wa pili mfululizo.

Aidha Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika kesho ijumaa katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Raisi wa Zanzibar Dk.Ally Mohammed Shein.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment