Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imesema inaunga mkono mkakati uliotangazwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wa serikali kutumia mtindo mpya wa utendaji kazi ambao uliwahi kutumiwa na nchi ya Malaysia na kuwapatia mafanikio makubwa kiuchumi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Godfrey Simbeye amewaambia Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, baada ya kukamilika kikao cha wanachama wa TPSF wa mikoa ya Dar es salaam,Lindi, Mtwara na Zanzibar, ambacho kilikuwa kinafanya maandalizi ya uchaguzi wa kupata bodi mpya.
![]() |
| Godfrey Simbeye - Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania |
Naye Mjumbe wa bodi ya TPSF, Arnold Kileo ambaye pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa taasisi hiyo, amesema mtindo huo mpya utaleta tija kubwa kiuchumi na ambao unaendeshwa na sekta binafsi.
![]() |
| Arnold Kileo - Mjumbe wa Bodi ya TPSF |



0 comments:
Post a Comment