Balozi wa China Tanzania Lu Yuoqing ameanza ziara yake ya siku tatu katika wilaya za Songea na Mbinga mkoani Ruvuma, ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kusaidia uwekezaji na watalaamu wa kilimo katika kuendeleza zao la Mahindi mkoani humo ili liweze kuingia kwenye mfumo wa kibiashara na kuuzika nje ya nchi.
 |
Lu Yuoqing - Balozi wa China Tanzania Balozi Lu Youqing ambaye amewasili jana mjini Songea kwa mwaliko wa Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenister Mhagama ameanza kwa kutembelea Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma pamoja ofisi ya wilaya ya Songea na kupokea taarifa ya wilaya hiyo ambayo inaanisha changamoto ya mapato kidogo yanayotokana na kutegemea ushuru wa asililimia 65 ya mazazo kuhudumia jamii. |
Balozi YOUQING amesema ili kukuza kipato cha halmashauri hiyo, Nchi ya China imeshatambua mashirikiano yake na mkoa wa Ruvuma hivyo itahakikisha inaleta wawekezaji na wataalamu wa kutosha kwa lengo la kuendeleza zao la Mahindi na kuliweka katika mfumo wa kibiashara zaidi na kuuza nje ya nchi.
 |
| Jenister Mhagama - Mbunge wa jimbo la Peramiho. |
Katika ziara hiyo walitiliana saini na shule ya sekondari ya Namihoro katika kudumisha ushirikiano wao na kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kutatua tatizo la vitabu na bweni katika shule hiyo huku Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama akiwataka wananchi kutulia na kupuuza wanaobeza maendeleo.
Balozi YOUQING amekabidhi Cherehani 20 kwa vikundi vya akina mama pamoja na baiskeli 20 kwa viongozi wa umoja wa vijana wa CCM wa kata zote za jimbo la Peramiho.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment