Sherehe za kuapishwa
kwa rais Uhuru Kenyatta zimefanyika kwa shangwe na nderemo mbele ya marais wa
nchi za Afrika, hata hivyo vingozi wa nchi za magharibi hawajahudhuria sherehe
hizo kutokana na aibu juu ya mashtaka dhidi ya Bwana Kenyatta na makam wake Willaim
Ruto dhidi ya uhalifu wa kibinadamu na ushirika wao katika madai ya unyanyasaji
baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
|
Uhuru Kenyatta wakati wa kula kiapo
|
Mbele ya halaiki ya
watu Uhuru Kenyatta ameapa akisema kwamba: “Mimi Uhuru Kenyatta, nafahamu uzito
wa majukumu yangu kama Rais wa Jamhuri ya Kenya, Naapa uaminifu na utii kwa
Jamhuri ya Kenya,"mkewe Margaret,
akishikilia Biblia ambayo aliyowekea mkono kwa kula kiapo kitabu ambacho hicho
hicho ndicho alichoshikilia hayati baba yake Jomo Kenyatta wakati wa kuapishwa
kwake kama rais wa kwanza mwaka 1964.
Rais mpya pia aliahidi
"kulinda na kutetea uhuru, uadilifu na hadhi ya watu wa Kenya,"
wakati wa sherehe za kuapishwa kwake zilizokuwa chini ya ulinzi mkali.
Uhuru Kenyatta mwenye
umri wa miaka 51 anakuwa rais wa kwazna mwenye umri mdogo nchini Kenya na wa
kwanza kuchaguliwa licha ya kuwa na keshi ya kujibu kwenye mahakama ya uhalifu
wa kivita ya ICC.
Makam wake wa rais
William Ruto ambae pia anashtakiwa na mahakama hiyo ya ICC kutoka jamii ya wa
Kalenjin alikua kiapo pia kushika hatamu ya uongozi.
Mgeni wa heshima
katika sherehe, Rais wa Uganda Yoweri kaguta Museveni amewapongeza wa Kenya
kutupilia mbali vitisho na vitimbi vya mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC kwa
kumchaguwa Uhuru Kenyatta kuwa rais wa jamuhuri ya nne ya Kenya.
Akizungumza katika sherehe za kuapishwa kwa rais
Uhuru Muigaye kenyatta kama Rais na William Samoe Ruto waliochaguliwa katika
uchaguzi mkuu nchini Kenya na ambao wanatakiwa kiripoti katika mahakama ya
uhalifu wa kivita ya ICC Julay 9 baada ya tuhuma za kuhusishwa katika mauaji ya
baada ya uchaguzi ya mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya elfu moja walipoteza
maisha huku watu kadhaa wakiyatoroka makwao.

0 comments:
Post a Comment