Image
Image

EXCLUSIVE: JESHI LA POLISI NCHINI LINAWASHIKILIA WATU 5 KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MWENDESHA BODA BODA MBEZI BEACH.


Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa watano akiwemo askari mgambo mmoja na wanajeshi  wanne kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwendesha bodaboda aliyeuawa maeneo ya Mbezi Beach na Kutupwa kando yam to.

ACP Charles Kenyela -Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondon 

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni ACP Charles Kenyela, amesema kuwa watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa watafikishwa mahakamani muda wowote kwa tuhuma za mauaji.

Amesema jeshi hilo linawashikilia watu 12 kwa tuhuma za kufanya fujo, kujeruhi askari watatu kwa mawe, kuharibu mali pamoja na kushambulia kituo cha Polisi cha kawe kwa madai ya kutaka kuwatoa watuhumiwa waliokuwa wanadaiwa kumuua dereva wa boda boda.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment