Image
Image

EXCLUSIVE: JUMUIA YA KIMATAIFA YATOA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA THATCHER.


Viongozi wa nchi na mashirka mbalimbali ya kimataifa yametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher mwenye umri wa miaka 87, ambaye alifariki jana asubuhi kutokana na ugonjwa wa kiharusi.
Margaret Thatcher - waziri mkuu wa zamani wa Uingereza.
Waziri mkuu wa Uingeraza David Cameron amesema, bibi Thatcher atakumbukwa kutokana na umahiri wake katika siasa na ameifanya Uingereza isimame tena.
Hivyo raia wa Uingereza hawana budi kumheshimu na kumshukuru.
Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Thatcher.
Katika salamu zake za rambirambi, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema, bi Thatcher ni mfano wa kuigwa na wanawake wengine duniani.
Serikali ya Uingereza inasema, mazishi ya bi Thatcher yatafanya tarehe 17 Aprili katika kanisa ya St Paul's. Serikali hiyo imeongeza kuwa, mazishi ya Bi Thatcher yatapewa hadhi sawa na mama wa malkia Elizabeth II na Princess Dianna.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment