Image
Image

EXCLUSIVE: MARIO BALOTELLI AFUNGIWA MECHI TATU, PAMOJA NA KOSA LA KUMKASHFU MUAMUZI.



STRAIKA wa AC MILAN, Mario Balotelli, amefungiwa jumla ya Mechi 3 baada ya kulimbikiza Kadi za Njano 5 na pia kuwakashifu Waamuzi wa Mechi dhidi ya Fiorentina iliyochezwa Jumapili iliyopita.

Wakati tayari akisubiri kuanza kutumikia Kifungo cha Mechi moja kwa kulambwa Kadi ya Njano ya 5 tangu aanze kuichezea AC Milan Mwezi Januari, Balotelli ameongezewa Kifungo cha Mechi mbili zaidi kwa kuwatukana Waamuzi wa Mechi hiyo na Fiorentina ambayo ilimalizika kwa sare ya Bao 2-2.
Mario Balotelli
Kifungo hiki kitamfanya azikose Mechi za Ligi za Serie A dhidi ya Napoli Wikiendi ijayo na zile na Juventus na Catania ambazo zitafuatia.

Mbali ya Kifungo hiki toka Chama cha Soka, Balotelli pia ana adhabu toka Klabuni kwake kwa kufumwa akivuta Sigara chooni ndani ya Treni iliyokuwa ikiwapeleka kwenye Mechi huko Florence.

Kuhusu Kifungo cha Mechi 3, AC Milan imethibitisha itakata Rufaa kupinga adhabu hiyo.

AC Milan inakamata nafasi ya 3 kwenye Serie A wakiwa Pointi 4 nyuma ya Napoli ambao wako Pointi 9 nyuma ya Vinara Juventus.

Kwa Mwaka 2013, Balotelli amepachika Bao 10 katika Mechi 11 alizochezea AC Milan na Timu ya Taifa ya Italy.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment