Image
Image

PHIL NEVILLE KUONDOKA EVERTON


NAHODHA na Beki wa Everton, Phil Neville, ataondoka Klabu hiyo mwishoni mwa Msimu huu.

Mchezaji huyo wa zamani wa England na Manchester United, mwenye Miaka 36, Mkataba wake na Everton unamalizika Juni 2013 na hataongeza Mkataba huo lakini hajatangaza kustaafu.

Phil Neville
Phil Neville ametamka: “Nataka kuendelea kucheza Soka katika ngazi ya juu kwa muda mrefu zaidi kadri inavyowezekana na nitakaa nitafakari nini cha kufanya.”

Msimu huu, Phil Neville, ameichezea Everton Mechi 25 ikiwa ni sehemu ya Jumla Mechi 303 alizoichezea Klabu hiyo na kwenye Ligi Kuu amecheza zaidi ya Mechi 500 zikiwemo zile alipokuwa Man United.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment