Image
Image

EXCLUSIVE: UJUMBE WA SHIRIKISHO LA KIMATAIFA LA MPIRA WA MIGUU FIFA KUWASILI, KUSHUGHULIKIA SAKATA LA UCHAGUZI MKUU WA TFF.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utawasili nchini Jumatatu (Aprili 15 mwaka huu) kwa ajili ya kushughulikia mchakato wa uchaguzi mkuu wa TFF.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Angetile Osiah amesema taarifa kutoka FIFA, ujumbe huo utaongozwa na Mkuu wa Idara ya Uanachama ya FIFA, Primo Covarro na utafanya kazi kwa siku tatu kuanzia siku ya ujio na kuondoka Aprili 18 mwaka huu.
Angetile Osiah -Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania  
Ujumbe huo ukiwa nchini, utakutana na wagombea uongozi walioathiriwa na uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ambao waliomba mashauri yao yaangaliwe upya, wagombea ambao walikata rufani FIFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kamati ya Rufani na Uongozi mzima wa TFF.

Hata hivyo  Angetile ameongeza kwamba Wajumbe hao wangependa kukutana na Waziri anayehusika na michezo, hivyo TFF imeiandikia Wizara ikipendekeza kuwa ujumbe huo ukutane na Waziri na wakuu wengine wa michezo Aprili 16 mwaka huu kabla ya kuanza kazi zao.

Aidha wagombea watakaosikilizwa na ujumbe huo wa FIFA ni pamoja na  Farid Salim Mbaraka Nahdi.Mbasha Matutu, Elliud Peter Mvella,Hamad Yahya,Michael Wambura na Jamal Emily Malinzi, ambaye alikuwa  Mgombea wa nafasi ya urais wa TFF aliyekuwa amepitishwa na Kamati ya Uchaguzi, lakini mwekaji pingamizi akakata rufani ambayo ilikubaliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF, hivyo kuondolewa kwenye mchakato, lakini akaomba shauri lake liangaliwe upya kwa kukata rufani FIFA.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment