Image
Image

EXCLUSIVE: TCU YAAGIZA KUFUNGWA KWA CHUO CHA TIU, KUTOKANA NA UDANGANYIFU.


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU imeuagiza Uongozi wa Chuo kinachojiita 'Tanzania International University (TIU)' kilichopo Kimara Matangini jijini Dar es salaam kukifunga mara moja Chuo hicho ikiwemo kusitisha haraka zoezi la udahili wa wanafunzi pamoja na mchakato mzima wa uanzishwaji wa chuo hicho kutokana na kufanya shughuli zake kinyume cha sheria zilizowekwa na TCU.
Prof. Magishi Nkwabi Mgasa - Katibu Mtendaji (TCU) 
Hayo yamebainishwa leo hii na  Katibu Mtendaji (TCU) Prof. Magishi Nkwabi Mgasa wakati wa mazungumzo yake na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam,  ambapo amesema  kuwa (TCU) haijatoa Ithibati kwa chuo hicho inayokiruhusu kudahili wanafunzi ambapo kimekuwa kikijitangaza kuwa kinatoa kozi ngazi ya vyeti, stashahada na shahada na kuwataka wananchi kuwa makini na vyuo vya namna hiyo vinapojitokeza ili kuepuka usumbufu.  
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo
Aidha licha ya kukifunga chuo hicho, kimetakiwa kuondoa mabango yote yanayokitangaza chuo hicho, pamoja na kurudisha gharama zote ambazo zimekwishatolewa na wanafunzi hao  walioanza zoezi la udahili, Sambamba na kuomba radhi kwa umma wa Watanzania na wadahiliwa kwa kuwadanganya kupitia vyombo vya habari.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment