Wanajeshi wa Umoja wa Ulaya wanaanza kuwapatia mafunzo wanajeshi wa Mali
katika wakati ambapo opereshini za kijeshi zinazoongozwa na Ufaransa
zinaendelea katika mji wa kaskazini wa Timbuktu .
Kouli Koro ni mji unaokutikana umbali wa saa moja kwa gari kutoka mji
mkuu wa Mali-Bamako.Huko ndiko wanajeshi wa Umoja wa Ulaya walikopiga
kambi yao-mbali kabisa na uwanja wamapigano,kaskazini ya Mali.Miongoni
mwa wanajeshi hao wa Umoja wa ulaya wanakutikana matabibu 40 wa kutoka
jeshi la Ujerumani Bundeswehr na waalimu 40 watakaosaidia kuwapatia
mafunzo ya kijeshi makuruti wa Mali.Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Thomas
de Maizière alipowatembelea wanajeshi wa Ujerumani alitoa wito kwa mara
nyengine tena wa kutolewa misaada kupambana dhidi ya wafuasi wa itikadi
kali ya dini ya kiislam kaskazini ya Mali:
"Ni kitisho kwa eneo lote la Sahel.Na Mali haiko mbali na bahari ya kati.Kwa hivyo ni kwa masilahi ya Ulaya pia kuhakikisha ugaidi hauenei nchini Mali."Amesema waziri wa ulinzi wa serikali kuu ya Ujerumani.
Jukumu la Wanajeshi wa Umoja wa Ulaya sio kupigana
Umoja wa Ulaya unapanga kuwapatia mafunzo wanajeshi 4000 wa Mali-wanajeshi wa Ujerumani wanawashughulikia mafundi.Dhahir ni kwamba tume ya Umoja wa Ulaya haitoshiriki katika mapigano na wakati wao umewekewa kikomo pia.Hata hivyo Umoja wa ulaya umejiachia uwezekano wa kurefusha muda ikihitajika:Mpango wa Umoja wa Ulaya umepangwa kuendelea kwa muda wa miezi 15.Viongozi wa serikali ya Mali wamedhamiria kuona muda huo haupindukii.Suala lakini ni kama utatosha?Itategemea kama ufanisi utakaopatikana utakuwa wa kutia moyo."
Serikali ya Mali inapendelea kuona juhudi za Umoja wa Ulaya zikileta tija haraka.Waziri wa ulinzi wa Mali Yamoussa Camara anasema anataraji vikosi vyao vya usalama vitaweza haraka na kwa ufanisi kuyakomboa haraka maeneo pamoja na kudhamini usalama na kushiriki katika meza ya mazungumzo.
Umoja wa ulaya ndio unaoshinikitza mazungumzo yafanyike pamoja na
makundi ya upande wa upinzani.Waziri wa ulinzi wa serikali kuu ya
Ujerumani anasema mazungumzo hayo ni sehemu ya utaratibu wa kuleta
suluhu ambao siku za mbele utayajumuisha pia makundi ya kaskazini ya
Mali.Utaratibu huo ni pamoja na kuitishwa uchaguzi Julai mwaka huu.
"Ni kitisho kwa eneo lote la Sahel.Na Mali haiko mbali na bahari ya kati.Kwa hivyo ni kwa masilahi ya Ulaya pia kuhakikisha ugaidi hauenei nchini Mali."Amesema waziri wa ulinzi wa serikali kuu ya Ujerumani.
| WANAJESHI WA MALI WAKIWA WAMEBEBA MABEGI WAKISUBIRI KUPATIWA MAFUNZO YA KIJESHI. |
Jukumu la Wanajeshi wa Umoja wa Ulaya sio kupigana
Umoja wa Ulaya unapanga kuwapatia mafunzo wanajeshi 4000 wa Mali-wanajeshi wa Ujerumani wanawashughulikia mafundi.Dhahir ni kwamba tume ya Umoja wa Ulaya haitoshiriki katika mapigano na wakati wao umewekewa kikomo pia.Hata hivyo Umoja wa ulaya umejiachia uwezekano wa kurefusha muda ikihitajika:Mpango wa Umoja wa Ulaya umepangwa kuendelea kwa muda wa miezi 15.Viongozi wa serikali ya Mali wamedhamiria kuona muda huo haupindukii.Suala lakini ni kama utatosha?Itategemea kama ufanisi utakaopatikana utakuwa wa kutia moyo."
Serikali ya Mali inapendelea kuona juhudi za Umoja wa Ulaya zikileta tija haraka.Waziri wa ulinzi wa Mali Yamoussa Camara anasema anataraji vikosi vyao vya usalama vitaweza haraka na kwa ufanisi kuyakomboa haraka maeneo pamoja na kudhamini usalama na kushiriki katika meza ya mazungumzo.
![]() |
| WANAJESHI WAMALI WAKIWA TAYA KUPATIWA MAFUNZO YA KIJESHI |

0 comments:
Post a Comment