Image
Image

EXCLUSIVE: MWAKYEMBE KUWA MGENI RASMI BONANZA LA WAANDISHI HABARI MWAKA HUU.

DK. HARRISON  MWAKYEMBE

Chama cha waandishi wa habari za michezo nchini Tanzania (TASWA) kimesema katika bonanza la mwaka huu la vyombo vya habari, mgeni rasmi katika bonanza hilo atakuwa Waziri mwenye dhamana ya Uchukuzi Dk. Harrison Mwakiembe.


Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Taswa Juma Pinto, ambapo amesema lengo la kumwalika Mwakyembe nikwaajili ya kuweza kutoa zawadi za vikombe na medali kwa waandishi watakao ibuka washindi siku hiyo pamoja na kuzungumza na washiriki wa bonanza hilo.

Bonanza la mwaka huu litakuwa bonanza la tofauti na miaka iliyopita, kwa kuwa litashirikisha sekta mbali mbali katika tasnia hiyo ya habari, Ikiwemo afya, uchumi, siasa, Pamoja na michezo, ili kufanya kila mmoja afurahie kutokana na bonanza hilo kuwa linafanyika Mara moja kwa mwaka kwa hiyo ni nafasi ya kipekee.
Amesema bonanza la mwaka huu litahusisha wadau  1500 kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini, huku kukiwa na burudani ya muziki, ambapo siku ya  Alhamisi Aprili 4,2013 saa tano asubuhi kutakuwa na mkutano na wanahabari mgahawa wa City Sports Lounge, Posta Dar es Salaam ambao ni maalum kutangaza makundi yatakayotumbuiza kwenye Media Day na tunatarajia makundi hayo nayo yatakuwepo kwenye mkutano huo.

Hata hivyo  ameviomba vyombo vya habari ambavyo havijathibitisha ushiriki wao kwa njia ya maandishi vifanye hivyo kama vilivyoagizwa kwenye barua zao za mialiko, vinginevyo ushiriki wao hautathaminika.
Aidha bonanza hilo litafanyika Jumamosi wiki hii viwanja vya Sigara, Chang’ombe, Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa moja usiku likidhaminiwa na na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment