Zaidi
ya watoto elfu kumi walio na umri kati ya miezi 3 hadi miaka 5 wamepatiwa
matibabu bure kutoka vijiji 16 vya Wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
Mapema leo mkurugenzi wa Kuratibu na
Kukuza Utafiti kutoka NIMR, Dk. Julius Massaga amesema zoezi hilo limefanikiwa
kupitia wahudumu wa afya za Msingi na lilikuwa likiwahusu zaidi watoto
waishio katika maeneo ambayo upatikanaji wa huduma za afya ni duni.
Dk. Julius Massaga - Mkurugenzi NIMR |
Kauli
hiyo imetolewa wakati wa Mkutano wa 27 wa Taasisi ya Taifa ya utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR) unaofanyika sambamba na na Kongamano la
pili la Wanasayansi watafiti barani Afrika, kwa siku nne jijini Arusha
Tanzania.
Dkt.Massaga
amesema watoto hao wamefaidika kwa kupatiwa matibabu bure kupitia mradi
unaoendeshwa chini ya NIMR ambao umelenga kupambana na kuepusha vifo
vinavyotokana na Malaria ndani ya Wilaya ya Pangani.
NIMR
ilitoa mafunzo na vifaa kwa wahudumu wa Afya 59 lakini kwa uchache wao wameweza
kuleta mafanikio kwa mradi huo na jamii kwa ujumla.
Awamu
ya pili ya mradi huo inataraji kuanza mwezi Mei 2013 hadi Mei 2014 na utasaidia
pia kutoa elimu dhidi ya Malaria kwa kaya mbalimbali.
Watafiti wanasayansi zaidi ya 300 wa magonjwa ya binadamu na wanyama kutoka Tanzania na nchi mbalimbali duniani wanashiriki kongamano hilo na mada 174 zinawasilishwa na kati ya mada hizo 42 zinajadili umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta za Afya,Mifugo,Wanyapori na Mazingira katika kuthibiti magonjwa ya mlipuko.

mbiu ya Kongamano hilo la pili barani Afrika la Afya moja ni Mabadiliko ya
mandhari ya tafiti za afya barani afrika.
0 comments:
Post a Comment