Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema nchi yake itatoa fedha nyingine za dola milioni 123 za kimarekani kwa wapinzani wa Syria kwa ajili ya misaada isiyokuwa silaha.
John Kerry - WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI
|
Ahadi hiyo ya Kerry ambayo itafanya nchi hiyo itoe jumla ya dola milioni 250 za kimarekani, imetolewa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mara tu baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi za magharibi na kiarabu huko Istanbul .
Msaada wa Marekani utalenga kutoa chakula na huduma za matibabu, pamoja na kuwasaidia viongozi wa Syria kufanya kazi kwa ajili ya kuleta demokrasia.
Aidha msaada huo kwa mara ya kwanza unatarajiwa kujumuisha magari ya kivita, mavazi ya kivita, miwani ya kuonea usiku na vifaa vingine vya kujilinda kijeshi.
Zaidi ya watu 70,000 wameuawa na zaidi ya milioni 1.3 wamekuwa wakimbizi na kukimbilia nchi jirani, tangu mgogoro wa Syria uanze miaka miwili iliyopita.
0 comments:
Post a Comment