Image
Image

EXCLUSIVE: IDADI YA VIFO YAONGEZEKA NA KUFIKIA 184 KUTOKANA NA TETEMEKO LA ARDHI CHINA

Takwimu mpya zilizotolewa na wizara ya mambo ya kiraia ya China zinaonesha kuwa, hadi sasa watu 184 wamefariki, 24 hawajulikani mahali walipo, na wengine 11,826 hivi kujeruhiwa.
Hata hivyo huenda idadi hiyo ikaongezeka kwani zoezi la uokoaji bado linaendelea kwenye sehemu zilizoathiriwa na maafa hayo.

wizara ya mambo ya kiraia imepeleka vifaa vya msaada kwenye eneo lililokumbwa na tetemeko vikiwemo mahema 30,000, mablanketi ya sufi 50,000 na vitanda vya muda 10,000.

Kikosi cha kazi chenye maofisa kutoka wizara nane zikiwemo mambo ya kiraia, afya, na mawasiliano wamekwenda moja kwa moja kwenye eneo lililokumbwa na tetemeko kufanya kazi ya kutoa msaada mapema jana.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment