Image
Image

EXCLUVE: WAZIRI KUU WA ZAMANI WA UINGEREZA MARGARET THATCHER AFARIKI DUNIA.

Margaret Thatcher enzi za uhai wake.

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87 kutokana na shinikizo la damu lililopelekea kupata mshtuko wa moyo.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na msemaji wa kiongozi huyo wa zamani Lord Tim Bell “ Ni kwa uchungu mkubwa Mark na Carol Tatcher wanatangaza kifo cha mama yao Margaret Tatcher aliefariki kutokana na mshtuko wa moyo.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na waziri mkuu wa sasa wa Uingereza David Cameron ambae anatoka chama kimoja na hayati huyo cha kihafidhina amesema wamempoteza kiongozi shupavu, kabla ya kutangaza kusitisha ziara yake barani Ulaya na hatimaye  kurejea kuomboleza.

Kwa upande wake Malkia Elizabeth II katika taarifa iliotolewa kutoka Buckingham ameonyesha  kusikitishwa na kifo cha kiongozi huyo wa zamani,  na ametuma salam za rambi rambi kwa familia.

Margaret Thatcher ndiye mwanamke pekee ambaye ameshawahi kuwa waziri mkuu nchini Uingereza katika karne hii ya XX, na alikuwa hajaonekana hadharani kwa kipindi cha muda mrefu, tangu mwaka 2002 kufuatia ushauri wa madactari na kutokana na kupata mshtuko wa mara kwa mara.
 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment