Bosi wa 'kru' ya MMG, Rick Ross, amemchagua rasmi mnyamwezi Kendell
Freeman p.k.a. Young Sav kuwa kama msaidizi wake - Vice Persident wa
lebo yake ya MMG.
Mkali huyu amekuwa na mchango mkubwa sana katika muziki wa Rick Ross,
na katika profile yake, amekwishapiga kazi ya nguvu na wakali kama
vile Lil' Jon, Pitbull, na Ying Yang Twins, Young Sav pia akiwa chini
ya lebo ya Def Jam kama Mixshow Manager, amepata nafasi ya kufanya kazi
kwa karibu na Jay-Z akiwepo pia Rick Ross, 2 Chainz, Fabolous na
Jadakiss.
Ross amesema anajisikia poa sana kuwa na
mtu kama Young Sav ndani ya Maybach Music Group, na kwa upande wake the
new Vice President - Amemshukuru sana Ross kwa kuona jitihada zake na
kumuweka katika nafasi kubwa kama hii.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment