Taarifa ya mtangazaji wa Radio One na ITV Reuben Mchome kupitia mchomeblog.com
imesema kuwa ajali hiyo ilitokea Mto Wami baada ya tela la lori hili
la mafuta kukatika na kuponea kwa asilimia ndogo sana kuzama kwenye mto
huo ambao kwenye ripoti kadhaa umeripotiwa kuwa na Mamba.
Hata hivyo inaelezwa kuwa mpaka lori hilo linaondolewa
kwenye eneo la ajali, maelfu ya abiria walikwama kwa muda wa zaidi ya
saa sita ambapo kwa pande zote mbili watu walilazimika kusubiri, huku
foleni ilikuwa ikionekana kubwa.
Aidha mwaka jana kulikua na taarifa
ya lori la mkaa kugonga kuta za mto huo na kuzama huku likiwa na
kondakta wake pamoja na dereva waliodaiwa kufariki.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)




0 comments:
Post a Comment