![]() |
| Uhuru Kenyatta. |
Uhuru Kenyatta anajiandaa kuapishwa rasmi leo kuwa rais
wa awamu ya nne nchini Kenya,
takriban miaka hamsini baada ya baba yake Jomo Kenyatta, rais wa kwanza wa Kenya huru.
sherehe za kula kiapo zinafanyika leo 9 Aprili, Marais wasiopungua kumi
na tano kutoka barani Afrika na wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya nchi za
Magharibi wanataraji kuhudhuria sherehe hizo, ambapo hata hivyo Uhuru Kenyatta
na naibu wake William Ruto wanakesi ya kujibu kwenye mahakama ya kimataifa ya
uhalifu wa kivita ya ICC baada ya kuhusishwa katika vurugu za baada ya uchaguzi
mwaka 2007.
Wa
Kenya wa tabaka mbalimbali wameanza kumiminika katika uwanja wa michezo wa
Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi,
tayari kushuhudia kuapishwa rasmi kwa rais mteule Uhuru Kenyatta na naibu wake
Wiliam Ruto. Marais takriban 15 pamoja na mabalozi spesheli 20 wanatarajiwa
kuhudhuria sherehe hizo.
Miaka mitano baada ya kushuhudia uchaguzi uliogubikwa na machafuko yaliogharimu maisha ya watu zaidi ya elfu moja, lakini kwa sasa taifa la Kenya limepiga hatuwa ya Demokrasia. Uhuru Kenyatta alichaguliwa katika duru la kwanza la uchaguzi na kura ndogo zaidi ya mpinzani wake Raila Odinga kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura.
Matokeo hayo yalipingwa na mrengo wa muungano wa Cord unaongozwa na Raila Odinga na kupekeleka kesi mahakamani, kesi ambayo baada mahakama ilitupilia mbali na kumtaja Uhuru Kenyatta kama mshindi halali katika uchaguzi uliofanyika Marchi 4, na Raila Odinga kukiri kushindwa na kukubali matokeo.
Katika uchaguzi wa mwaka 2007 baada ya Raila Odinga kutangazwa kuwa ameshindwa kwenye uchaguzi na Mwai Kibaki na baaae kuzuka machafuko ya umwagaji mkubwa wa damu kuwahi kutokea katika Historia ya Kenya.

0 comments:
Post a Comment