Image
Image

VIGOGO WATATU WIZARA YA ARDHI KIZIMBANI.

VIGOGO watatu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka manne, ikiwamo la matumizi mabaya ya madaraka, ufujaji na ubadhirifu wa fedha na wizi wa Sh200 milioni.
Waziri wa ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka.
Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sera na Mipango, Simon Lazaro, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa Ardhi, Mipango na Matumizi, Gerald Mango na Kaimu Mhasibu Mkuu  wa NLUPC, Charles Kijumbe.

Katika shtaka la kwanza linalomkabili  Simon, Swai alidai kuwa  Novemba 17, 2012 katika ofisi za Kamishna wa Ardhi, Mipango na Matumizi iliyopo Wilaya ya Ilala aliwasilisha  nyaraka  za marejesho ya matumizi ya fedha kwa Mkurugenzi w wa Tume ya Ardhi Mipango na Matumizi akionyesha Sh100 milioni zilipokelewa kwa ajili ya matumizi ya mipango na matumizi ya ardhi wilaya za Babati, Kilolo  na Bariadi  wakati akijua kuwa siyo kweli.

Swai alidai katika shtaka la pili, washtakiwa wote kati ya Julai 2011 na Agosti 5, 2011 wakiwa waajiriwa wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi, walitumia madaraka yao vibaya kinyume na kanuni ya  87 (1) na 86(1)  ya Sheria ya Udhibiti wa Fedha za Umma  ya 2004. Katika washtakiwa walikana mashtaka yote yanayowakabili, Hakimu Katemana aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 30, mwaka huu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment