Mjukuu wa
Marehemu Bi Kidude Amesema bibi yake amefariki leo nyumbani kwa mtoto wa kaka
yake katika maeneo ya bububu.
Marehemu Bi Kidude/ Picha hii ni Enzi za Uhai wake wakati akiwa anasumbuliwa na Maradhi. |
Amebainisha
hayo mda mfupi mara baada ya baadhi ya wanahabari kutaka kufahamu kwa kina juu ya
habari za msiba huo wa ulio stua uma wa watanzania na watu wengine wanao
mfahamu na kutambua kitu gani alichokuwa akikifanya katika mziki nchini na nje
ya nchi, Ambampo fatma ambaye naye ni mwimbaji amekiri kuwa bi kidude ni kweli
kafariki dunia na taratibu za Mazishi bado zinaendelea kufanyika huku mwili wa
marehemu ukihamishiwa kupelekwa nyumbani kwake Raha leo.
Sijambo geni
kusikia kuzushiwa kufa kwa bi kidude ambaye kwa sasa hatunaye tena, lakini
kwasasa amesema kuwa kwa 100% ni ukweli na siuzushi juu ya habari za kufariki
kwa nguli wa muziki wa Taarabu nchini Tanzania.
Anasema Bi
kidude alianza kusumbuliwa na marahi mapema mwaka jana, lakini baada ya muda
alipata ahueni, lakini ghafla mambo yakabadilika na hadi kupata umauti.
0 comments:
Post a Comment