Image
Image

ZOMBE KUTINGA MAHAKAMANI KESHO

MKUU wa Upelelezi wa mkoa wa Dar es Salaam (RCO) wa zamani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na wenzake wanane,
waliokuwa wakikabiliwa na mauaji ya wafanyabiashra wa madini kutoka Mahenge Morogoro kesho wanatinga tena mahakamani, wakati rufaa yao itakaposikilizwa na Mahakamka ya Rufani.


(ACP) Abdallah Zombe
Zombe na wenzake walikuwa wakidaiwa kuwaua Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi Juma Ndugu, katika msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis, Jijini Dar es Salaam, Januari 14, 2006. Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote Mahakama Kuuu Kanda ya Dar es Salaam , Agosti 17, 2009, ikisema kuwa upande wa umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao bila kuacha mashaka yoyote, na hivyo hawana hatia
Hata hivyo , Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alikata rufaa Mahakama ya Rufani, kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, akidai kuwa Jaji Salum Massati alikosea kuwaachia huru washtakiwa hao, akidai kuwa kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani. Rufaa hivyo imepangwa kusikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, leo na kesho. Jopo la majaji hao linaongozwa na Jaji Edward Rutakangwa, akisaidiana na Jaji Bernard Luanda na Jaji Salum Mbarouk.  


Katika rufaa hiyo namba 254/2009, iliyofunguliwa mahakamani hapo Oktoba 6, 2009, DPP amebainisha sababu 11 ambazo zimemfanya apinge hukumu hiyo yote, akidai kwamba kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani, washtakiwa wote walikuwa na hatia. Mbali na Zombe, wajibu rufaa wengine ni ASP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, Konstebo Jane Andrew, Konstebo Emanuel Mabula, Konstebo
Michael Shonza, Koplo Abeneth Salo, Koplo Rashid Lema, Koplo Rajabu Bakari na Koplo FestusGwabisabi
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment