Image
Image

JOTO LA PANDA UTEUZI WA MAWAZIRI KENYA

Nairobi,Kenya 

Kenyatta JOTO la Baraza la Mawaziri katika serikali mpya ya awamu ya nne ya Kenya inayongozwa na Rais Uhuru pamoja na makamu wake William Ruto imeanza kupanda.

Joto hilo la mawaziri limeanza kupata ikiwa ni siku tano tu baada ya wawili hao kutangaza muundo wa mabaraza jimpya na la kisasa kutoka na udogo wake ikiwa na mabaraza 18 tu ukilinganisha na la mtangulizi wake Mwai Kibaki iliyokuwa na mabara 44.

Uhuru Kenyatta - Rais wa Kenya
Kitendo cha Rais Kenyatta na makamu wake kutangaza muundo wa baraza hilo wiki moja iliyopita bila kuja majina ya mawaziri imeongeza wasiwasi kwa wakenya wengi pamoja na wabunge waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliopita Machi 4 mwaka huu.
Hata hivyo Makamu wa Rais Ruto amewai kunukuliwa kwenye vyombo vya habari akisema kwamba, baraza la mawaziri itaundwa na wanasiasa waliofanya vizuri zaidi katika uchaguzi huo  huku ikiwa na sura nyingi za wanawake.

"Hatutengenezi ajira za wanasiasa walioshindwa wala waliofana vibaya, ila tutakuwa na baraza la nawaziri wenye uwezo na watakao iletea taifa maendeleo, hivyo kila mtu atakaye pata nafasi ya kuingia kwenye baraza hilo atakuwa tayari kuwatumikia wakenya"alisema Ruto katika mahojiano yake na vyombo vya habari nchini Kenya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment