Leo nilipata nafasi ya kuzingumza na
Gadna G Habash ambaye ni Meneja na Mume wa Mwanamuziki maarufu nchini Lady Jay
Dee, sote tunafahamu juu ya maneno aliyoyasema Lady Jay Dee kama ni Wosia wake.
Kupitia kipindi cha The Takeover
kinachorushwa na kituo cha TBC fm haya ndio yalikuwa majibu ya maswali
niliyomuuliza Gada G;
Swali 1. Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa
Lady Jay Dee...?
Gadna G: Ni maneno ambayo yametoka moyoni mwake na ni maneno mbayo
anajitetea kama msanii, mimi kama Meneja ukiacha pia kama mke wangu naendelea
kumsapot kwa kile ambacho anaona ni sawa, basi mimi nitaendelea kumsaport na
kujaribu kuzungumza na Lady Jay Dee, mara nyingi anasema tu kwamba watu
wasifikilie ni swala la wimbo kupigwa au kutokupigwa, hayo ni mambo ya kawaida
lakini wafikirie tu kwamba huyu mtu anaongea kutokana experience yake aliyokuwa
nayo na wale watu.
Baada ya mwaka 2003 kuacha kufanya
kazi kwenye management yao ya Smooth Vibe, yalitokea mambo mengi hapa katikati
ila hakusema lakini siku za hivi siku za karibuni kuna mengine ambayo
yametokea, ndio akaona hapana nisipo sema nitazidi kukandamizwa na matokeo yake
nitakufa kisabuni.
Gadna G Habash |
Sawli 2. Hii ni kama vita mmejipangaje..?
Gadna G: Unapoamua kusema ukweli swala la kujipanga mara mbili huwa
halipo, ni kwamba unasema ukweli watu wasikie naukizungumzia uhasama watu
watauliza juu ya uhasama lakini ulikuwepo tayari kwahiyo tu watu wanajua kwa
sasa kwa kuwa jdee ameamuwa kuongea lakini tu hawajui tu kwamba jdee alikuwa na
matatizo na wale watu tangu kipindi cha nyuma sababu wale watu wanafumo dume ya
kufanya kazi na alipoachananao aliona kama wanamfatilia kulekule ambapo yeye
alipo.
Swali 3. Nini mlikiona kama chokochoko...?
Gadna G: Unajua kwa mfano unaweza kumuomba mtu maji akakwambia sina,
ukayaona yale pale ukamwambia niuzie akakuuzia ila bado alivyokuuzia akaona
kama unafaidi, mwisho akakwambia yameisha nenda sehemu nyingine, ukaenda sehemu
nyingine na ukayapata bure, akaona umepata akaamua kukufata kulekule na
akakukuta unakunywa maji kwenye grasi kisha akakuputa, sasa hapo inabidi useme
hapa unavyofanya sio sawa ndo hicho anachofanya Jay Dee sasa hivi.
Swali 4. Hali hii imewaathiri kwa kiasi
gani...?
Gadna G: Cha kushukuru Mungu ni
kwamba msanii au hata pia stesheni ya redio inategamea umma wa Watanzania au
hata mashabiki kwa ujumla kwa kuwepo kwake.
Jay Dee anapata saport nzuri kutoka
Watanzania, basi ujue hata hajaathirika chochote, na pia tu anaendelea kufanya
kazi kwa bidii, ila tu isipokuwa unapoona mtu anafanya madhara ili tu mtu apate
athari fulani ndio unasimama kuongea, ndiyo maana tuna Bunge na watu
wanasimama, watu wanaongea, watu wanatetea hoja, ndiyo maana yake. Yani lazima
mtu usimame useme ukweli kwa unalohisi hili jambo litanipa madhara nisiposema.
Swali 5. Kwa Wasanii wengine unawaambiaje...?
Gadna G: Uwoga ni kitu ambacho binadamu tumeumbiwa, wakati mwingine
unasaidia wakati mwingine unakudhiru uwoga wako,kwa sababu wanasema adui wa
maendeleo yako mwenyewe ni wewe mwenyewe, ndiyo maana uwoga wako unaeza
ukasabishwa ukakandamizwa zaidi, ndiyo maana wazee wetu waliweza kusimama na
kuikomboa hii nchi kwa sababu walisimama hawakuogopa.
Wangeogopa hii leo hii nchi
tusingekuwa huru, kwa hiyo kama kuna mtu ana jambo na anaogopa kusema hilo ni
jambo la kawaida kuogopa, lakini wakati wa kusema ukifika usiogope kusema ili
mradi useme ukweli, basi inatosha....
Swali 6. Kauli yako ya mwisho ni ipi..?
Gadna G: Ni kwamba wanahitaji kujua ukweli na kuambiwa ukweli, mtu
yoyote anayejua kitu cha kweli anaweza kusema sio sawa, utaendelea
kukandamizwa. Kauli ya mwisho ndo hiyo wanahitaji kuambiwa ukweli na kusikia
ukweli ili kama wanakosea wasiendelee kukosea wabadilikee….
Mwisho
Source: Gongamx
0 comments:
Post a Comment