Bwana shirima akiwa chini Baada ya Kudondoka juu ya Ghorofa |
Baadhi
ya mashuda ambao walikuwa katika eneo hilo walisema kuwa walishangaa kusikia
mlio uliokuwa na kishindo kama la tairi ya gari iliyo pasuka, ndipo ikawalazimu
kwenda kuangalia nini kimetokea ndipo walipo muuona mwanaume huyo akiwa kalala
chini, baada ya kujitupa toka juu hadi kuangukia tax iliyokuwa imepaki maeneo
hayo nakupondeka.
Takribani
dakika 30 ya watu waliokuwa wamefika katika eneo hilo kushuhudia kilicho tokea
walipatwa na bumbuazi, huku sinto fahamu ikiwa imegubika vichwa na midomo yao
kwa kilicho tokea pasi na matarajio yao.
Baada
ya kujaribu kumtafuta mtu atakayeweza kuzungumzia tukio hilo kwa undani juhudi
ziligonga mwamba, hiyo yote ni kutokana na kila mmoja kutotaka kuwashahidi wa
hilo na kilichotokea katika eneo hilo ikiwa bado nawao hawana ushahidi wa
kutosha.
Hata
hivyo Bado kiini haswa cha bwana shirima kujitupa toka ghorofani hadi chini
kimekuwa ni kitendawili miongoni wa watu walioshuhudia tukio hilo, ambapo
alionekana kupasuka sehemu ya paji la uso na kwenye kichwa huku damu zikiwa
zimechuruzika chini na watu wakiwa wamepoteza matumaini kwamba huenda akapona
ama la.
0 comments:
Post a Comment