Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana liliahirishwa
baada ya Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA) kukataa kuomba
radhi, Marekebisho ya hotuba ya upinzani kuhusu CUF na ushoga.
Haya
hapa Mabadiliko katika ukurasa wa 8 aya ya pili inayoanza na maneno ‘Mheshimiwa
Spika, Kwa upande wa chama cha CUF.... na kuishia na maneno… Israel Liberal ‘ sasa isomeke:
“Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha
CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali chama hicho ni mwanachama
wa Umoja wa Vyama vya Kiliberali Duniani (Liberal International).
Kwa mujibu wa tovuti ya umoja huo CUF
imejiunga na Oxford
Congress ya Liberal International Mwaka 1997.
Mwaka huo huo Liberal International ilitoa
msimamo wa pamoja wa umoja huo uliotwa Liberal Manifesto (Ilani ya Kiliberali)
ya 1997 iliyopitishwa katika mkutano mkuu wake wa 48 uliofanyika tarehe 27
mpaka 30 Novemba 1997 katika ukumbi wa Mji wa Oxford nchini Uingereza.
Katika ilani hiyo ya waliberali, umoja wa
vyama hivyo ulikubaliana msimamo wa pamoja, nanukuu: “the extension of the
rules of equality to sexual minorities and the recognition that homosexuality
and lesbianism are legitimate expressions of personal proclivities”.
Kwa
Tafsiri rahisi waliberali hao walipitisha ajenda ya waliberali katika karne ya
21 (The Liberal Agenda in the 21st Century) ya kuutambua ushoga na usagaji kama matendo halali.
Hii ni kwa mujibu wa tangazo la Umoja huo
kwenye mtandao wao wa waliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki
na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats
wakati chama hicho (Liberalism) kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa
za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja.
Kupitia umoja hao CUF
inashirikiana na vyama vingine kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre
cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel
Liberal………”
Ezekiah Dibogo Wenje
Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa
30 Mei 2013
0 comments:
Post a Comment