Baraza la
mitihani Tanzania,
leo limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika mwezi
February mwaka huu.
Akitangaza
matokeo hayo katika ofisi za baraza hilo
Mikocheni jijini DSM, Naibu katibu mtendaji wa baraza hilo Dr. Charles Msonde
amesema Jumla ya watahiniwa wa shule 40,242 kati ya watahiniwa 42,952 sawa na
asilimia 93.92 wamefaulu kwa daraja la 1 hadi la nne.
Aidha Dr msonde
ametaja shule 10 bora, zilizoongozwa na Marian Girls ya Pwani katika kundi la
watahiniwa zaidi ya 30 ambazo ni Mzumbe Secondary school, Feza Boys, Ilboru, Kisimiri,
St. Mary's Mazinde juu, Tabora Girls, Igowole, Kibaha Secondary school na
Kifungilo Girls.
Pia ametaja watahiniwa waliofanya vizuri katika
masomo mbalimbali, Kwa upande wa Sayansi aliyeongoza ni Erasmi Inyanse
aliyekuwa akisoma PCM kutoka Ilboru
0 comments:
Post a Comment