Serikali ya Misri imewakamata watu wawili
wanaotuhumiwa kuhusika na kutekwa nyara kwa askari 7 katika eneo la Green Valley,
kaskazini mwa Sinai.
Askari hao waliachiwa tarehe 22, Mei, siku sita baada ya
kutekwa.
Watuhumiwa hao wamekamatwa jana mjini Arish,
na wanatuhumiwa kuhusika na kutuma video ya askari waliotekwa nyara kwenye
mtandao siku mbili baada ya askari hao kutekwa.
Mohamed Morsi - Rais Misri. |
Video hiyo inawaonyesha askari
hao wakimtaka Rais Mohamed Morsi wa Misri kutekeleza masharti ya watekaji hao
ambao walimtaka rais huyo kuwachilia ndugu zao walioko gerezani kutokana na
kuhusika na mashambulizi ya kigaidi.
Msako wa kuwakamata watuhumiwa wengine wa
tukio hilo bado
unaendelea.
0 comments:
Post a Comment