Shirika la habari la Zimbabwe New Ziana
limesema, ziara ya rais Robert Mugabe wa nchi hiyo nchini Japan ni dalili
kuwa nchi hiyo inaanza kutoka kwenye kipindi cha kutengwa na nchi za magharibi.
ROBERT MUGABE |
Shirika hilo
limesema, rais Mugabe atahudhuria mkutano wa kimataifa wa Tokyo
kuhusu maendeleo ya Afrika utakaofanyika Yokohama
jumamosi hii. Hii ni mara ya kwanza kwa Zimbabwe kuhudhuria mkutano huo
tangu uanzishwe mwaka 1993.
Rais Mugabe ambaye yuko kwenye orodha ya
Marekani na Umoja wa Ulaya ya watu waliowekewa vikwazo, anatarajiwa kukutana na
waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, ambapo pia ni mara ya kwanza kwa rais huyo
kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na kiongozi wa nchi kubwa inayoegemea nchi
za magharibi.
Viongozi wa Zimbabwe
na Japan walikutana kwa mara ya mwisho mwaka 1989.
0 comments:
Post a Comment