Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini tanzania , Judith Wambura Maarufu kama Lady Jaydee ametangaza kuahirisha shughuli ya maadhimisho ya miaka 13 tangu aanze muziki iliyokuwa imapangwa kufanyika Ijumaa hii ya Mei 31, 2013 katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge kupisha shughuli za msiba wa vifo vya wasanii wawili Albert Robert Mangweha na M TO THE P waliofariki huko Afrika Kusini .
Amesema hayo muda mfupi uliopita (saa 3:52 asubuhi) wakati akihojiwa katika kipindi cha Super Mix ya East Africa Radio na mtangazaji Zembwela.
|
LADY JAYDEE - MWANAMUZIKI TANZANIA.
Jaydee ameeeleza uamuzi wake wa kusitisha show hiyo kuwa unalenga kutoa nafasi kwa wafiwa wote na wadau wa tansnia ya muziki na wapenzi wa Mangwea kumaliza taratibu za kumsitiri kipenzi chao na kueleza kwamba tarehe nyingine ya shughuli hiyo itatangazwa baadae.
|
Tangu amekaribishwa studio, Judith Wambura alionekana kuwa na majonzi kiasi cha kushindwa kuongea mara kwa mara na kukatisha mazungumzo yake kutokana na msiba wa wasanii hao.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment